Kikao kazi cha 4 cha Serikali Mtandao (e-GA)

Kikao kazi cha 4 cha Serikali Mtandao (e-GA) Kimeanza Leo Jumanne ya Februari 6,2024 hapa katika Ukumbi wa Simba-AICC, Arusha. Kikao hicho kimefunguliwa rasmi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene.

Wakati wa kikao hicho Mh.Simbachawene alisisitiza umuhimu wa Taasisi zote za Umma kufanya kazi zao kwa kutumia mifumo ya TEHAMA ili kutoa huduma bora na kwa wakati kwa Umma wa Watanzania.

Wajumbe zaidi ya 1300 wanahudhuria Kikao kazi hicho.

 

Facebook
X
LinkedIn

Event Booking Request